Luke 2:1-6

Kuzaliwa Kwa Isa

(Mathayo 1:18-25)

1 aSiku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 2 b(Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Shamu
Shamu inamaanisha Syria.
).
3Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

4 dHivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5 eAlikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. 6Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu wa kujifungua ukawa umetimia,
Copyright information for SwhKC